Mshambuliaji anayeminika kuwa kuwa ndiye nyota wa jezi namba 10 hapa nchini katika miaka ya 70, Maulid Dilunga wa Yanga alifanya kejeli dhidi ya mahasimu wao wa jadi Simba.
Dilunga alifunga goli kabla ya mapumziko katika mechi ya fainali ya klabu bingwa dhidi ya Simba ambapo matokeo hadi mapumziko yalikuwa Yanga 1-0.
Dilunga hakurudi uwanjani kipindi cha pili, badala yake alikwenda nyumbani kwa muda, kishaaliporejea uwanjani alikuwa amebadili mavazi na kuvaa suti. Mpira ulipomalizika, Yanga ilishinda 1-0.
Julai 20,1977- Kibaden apiga Hat-trick Yanga
Katika historia ya mapambano ya mahasimu wa jadi timu za Simba na Yanga, mchezaji aliyeweka rekodi ya kufunga magoli matatu katika mechi za mahasimu hao ni Abdallah 'King' Kibaden (Chief Mputa).
Kibaden aliweka rekodi hiyo katika mechi iliyochezwa Julai 20, 1977 kwenye uwanja wa Taifa (Uhuru).
Simba ilishinda 6-0, Kibaden alifunga magoli matatu dakika ya 25,40,44.
Abdallah Kibaden (katikati) akiwa katika benchi la wachezaji wa Simba katika moja ya mechi za timu hiyo miaka ya 90. Kulia ni Kocha Msaidizi Etinne Eshete na kushoto ni Daktari Msemakweli

Julai 20,1977- Simba 6 Yanga 0
Ilichukua miaka tisa timu ya Simba kulipiza kisasi cha magoli 5-0 dhidi ya Yanga katika mechi ya kuwania ubingwa wa Tanzana iliopigwa Jumanne Julai 20, 1977 kwenye uwanja wa Taifa (Uhuru).
Mahasimu hawa wa jadi walikutana na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0. Magoli yalifungwa na Abdallah Kibaden (dk 25,40,44), Selemani Saidi Sanga (beki wa kushoto wa Yanga aliyejifunga mwenyewe na (dk 30),Jumanne Hassan Macimental(dk 60,74).
Kikosi cha Simba:
Omary Mahadhi, Daudi Salum, Mohamed Kajole,Aloo Mwitu,
Mohamed Tall, Athumani Juma,Willy Mwaijibe, Aluu Ally, Jumanne Hassan,Abdallah Kibaden na Martin Kikwa/Abbas Dilunga.
Yanga: Yanga: Benard Madale, Charles Boniface, Selemani saidi, Mwanga,Freddy, Jongo, Sam Kampambe, Shabani Katwila, Ezekiel Greyson, Mwinda Ramadhan, Yanga Bwanga na Ayoub/Mrisho Caraby.

Yanga na Simba
Rekodi za kufungana magoli mengi mahasimu wa jadi Yanga na Simba katika historia ya timu hizo ni mbili tu. Nazo ni-
Juni 1,1968- Yanga 5 Simba 0
Yanga iliweka rekodi ya kuifunga magoli mengi Sunderland (Simba) Juni 1,1968 kwenye mchezo wa klabu bingwa ya nchi uliopigwa uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Simba ilifungwa 5-0, magoli ya Yanga yalifungwa na Maulidi Dilunga kwa njia ya penalti (dk 18,43), Salehe Zimbwe (dk 54,89),Kitwana Manara (dk 86).
Yanga ilimwazima Salehe Zimbwe toka Tanga na kumtumia Gilbert Mahinya wa Simba kutokana na wakati huo hakukuwa na kanuni ya usajili rasmi.

Unajua Chalenji ilikotokea?
Historia ya mashindano ya Kombe la Chalenji inayoshirikisha nchi za Afrika Mashariki na Kati ilianza mwaka 1926 wakati Tajiri, William Gossage aliyekuwa akimiliki kiwanda cha kutengeneza sabuni nchini Kenya, kutoa kombe la 'Ujirani mwema'lililoshindaniwa na nchi za Kenya na Uganda.
Tanganyika ilijiunga na mashindano hayo ya Gossage mwaka 1945 na kufuatiwa na Zanzibar mwaka 1949.
Nchi nyingine zilizojiunga na kombe hilo ni Malawi na Zambia ambazo hata hivyo zilijiondoa na kujiunga na Shirikisho la Vyama vya Michezo Kusini mwa Afrika (COSAFA) kwa madai kuwa nchi za Afrika mashariki zilikuwa na ushindani mdogo, tofauti na ushindani uliokuwepo kusini mwa Afrika.
Michuano hiyo iliendelea kuzivutia nchi za Ethiopia, Sudan na Somalia ambazo zilijiunga na kuifanya michuano hiyo kupanuka zaidi kutokana na nchi za Afrika Kati kuongeza nguvu.
Aidha, nchi za Rwanda, Burundi, Elitrea na Djibout nazo zilijiunga na kufikisha idadi ya nchi 12.

Subscribe to:
Posts (Atom)