Rekodi za kufungana magoli mengi mahasimu wa jadi Yanga na Simba katika historia ya timu hizo ni mbili tu. Nazo ni-
Juni 1,1968- Yanga 5 Simba 0
Yanga iliweka rekodi ya kuifunga magoli mengi Sunderland (Simba) Juni 1,1968 kwenye mchezo wa klabu bingwa ya nchi uliopigwa uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Simba ilifungwa 5-0, magoli ya Yanga yalifungwa na Maulidi Dilunga kwa njia ya penalti (dk 18,43), Salehe Zimbwe (dk 54,89),Kitwana Manara (dk 86).
Yanga ilimwazima Salehe Zimbwe toka Tanga na kumtumia Gilbert Mahinya wa Simba kutokana na wakati huo hakukuwa na kanuni ya usajili rasmi.