Nchi za Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda zilianza mchezo wa soka mwanzoni mwa mwaka 1920 baada ya Waingereza kuingia Afrika Mashariki wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia 1914 na Vita Kuu ya Pili 1945.
Dk Omari Ali Juma akipeana mkono na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hussein Masha wakati wa pambano la kirafiki la kimataifa na timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Lady JD ametokea wapi?
Jina lake halisi ni Judith Wambura Mbibo ni
mwanamuziki wa kike ambao kwa kiasi kikubwa wameweza kuteka hisia za mashabiki wengi wa muziki Afrika ya Mashariki na kati. Msanii huyu alizaliwa mkoani Shinyanga Juni 15 mwaka 1979 na safari yake ya muziki ilianzia kanisani, ambako ndiko kipaji chake kilianza kujionyesha akiwa binti mdogo kutokana na kuwa na sauti nzuri iliyokuwa ikiwasisimuwa waumini waliokuwa wakisikiliza nyimbo za kwa ya ambayo alikuwa akiimbia mwanamuziki huyo.
Baada ya kumaliza shule msanii huyu alianza kutangaza katika kituo cha redio cha Clouds FM, ingawa akaamua kuugeukia rasmi muziki mwaka 2000.
Mpaka sasa Jide ameshafanikiwa kutoa takriban albamu nne (4). Albamu yake ya kwanza aliita "Machozi" aliyoitoa mwaka 2000, "Binti" 2003, "Moto" 2005 na ya sasa ambayo ameipa jina la "Shukrani".
Msanii huyo aliyemaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya Zanaki alikuwa akifanya matamasha mbalimbali huku akiigiza nyimbo za wasanii mbalimbali wa muziki kama "Mc Lyte","Da Brat" ingawa katika kipindi hicho msanii huyu alikuwa akirapu zaidi kuliko kuimba.
Jide ambaye alianza kupanda jukwaani tangu alipokuwa sekondari lakini yeye mwenyewe anakiri kwamba mara yake ya kwanza kupanda jukwaani ilikuwa ni wakati wa ufunguzi wa shoo ya mwanamuziki Chaka Chaka pamoja na Brenda Fassie, wakati wanamuziki hao kutoka Afrika Kusini ambao walikuja hapa nchini katika nyakati tofauti tofauti.
Judith Wambura Mbibo au (Lady JD) akiwa katika moja ya shoo zake

1979- Simba katika maajabu ya Guiness
Timu ya Simba ilifanya maajabu ya kuingia katika kitabu cha Guiness na kuweka rekodi barani Afrika kwa kuifunga Mufurila Wanderers ya Zambia magoli 5-0 nyumbani kwao. Simba katika mchezo wa awali uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ilifungwa magoli 4-0 na Mufurila, hivyo kwenda Zambia ikiwa na matumaini finyu ya kupata ushindi. Mashabiki wengi walipendekeza timu hiyo isiende Zambia kwa hofu ya kipigo cha magoli mengi zaidi.
Simba ilikwenda Zambia kwa kutumia njia ya treni na katika pambano hilo la marudiano mgeni wa heshima alikuwa, Rais Kenneth Kaunda wa Zambia.
Magoli ya Simba yalifungwa na George Kulagwa dakika ya 12, Thuwein Ally dakika ya 19 na Abdallah Mwinyimkuu dakika ya 34. na hadi timu zinakwenda mapumziko Simba ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili Abbas Dilunga aliipatia Simba goli la nne dakika ya 59 na dakika ya 72 Abdallah Mwinyimkuu aliipatia Simba goli la tano .
Baada ya mchezo watanzania ambao walikuwa wakiishi Zambia waliamka vitini na kushangilia kwa nguvu zao zote. Mbali ya kushangilia huko Watanzania hao waliandaa pati iliyofanyika katika bar ya Mtanzania mwenzao Eddy Sally.
Kikosi cha Simba kilifundishwa na jopo la makocha akiwemo Joel Bendera ambaye kwa sasa makocha akiwemo, Joel Bendera ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Kikosi cha simba kilipangwa hivi: Athumani Mambosasa, Daudi Salum, Mohamed Kajole, Philbert Rubibira, Hussein Tindwa, Abbas Kuka, George Kulagwa, Abdallah Mwinyimkuu, Thuwein Ally, Ismail Mwarabu, Abbas Dilunga/Abdallah Hussein.

Subscribe to:
Posts (Atom)