TEMBELEA KILA WIKI, SOMA HABARI MPYA. USIKOSE MENGI MENGINEYO WIKI IJAYO. TUPO MAHIRI KUKUHABARISHA PATA VITU VIPYA HAPA. PATA BURUDANI ,HADITHI NA MATUKIO YA MICHEZO KILA JUMA.

Lady JD ametokea wapi?

Jina lake halisi ni Judith Wambura Mbibo ni
mwanamuziki wa kike ambao  kwa kiasi kikubwa wameweza kuteka hisia za mashabiki wengi wa muziki Afrika ya Mashariki na kati. Msanii huyu alizaliwa mkoani Shinyanga Juni 15 mwaka 1979 na safari yake ya muziki ilianzia kanisani, ambako ndiko kipaji chake kilianza kujionyesha akiwa binti mdogo kutokana na kuwa na sauti nzuri iliyokuwa ikiwasisimuwa waumini waliokuwa wakisikiliza nyimbo za kwa ya ambayo alikuwa akiimbia mwanamuziki huyo.
Baada ya kumaliza shule msanii huyu alianza kutangaza katika kituo cha redio cha Clouds FM, ingawa akaamua kuugeukia rasmi muziki mwaka 2000.
Mpaka sasa Jide ameshafanikiwa kutoa takriban albamu nne (4). Albamu yake ya kwanza aliita "Machozi" aliyoitoa mwaka 2000, "Binti" 2003, "Moto" 2005 na ya sasa ambayo ameipa jina la "Shukrani".
Msanii huyo aliyemaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya Zanaki alikuwa akifanya matamasha mbalimbali  huku akiigiza nyimbo za wasanii mbalimbali wa muziki  kama "Mc Lyte","Da Brat" ingawa katika kipindi hicho msanii huyu alikuwa akirapu zaidi kuliko kuimba.
Jide ambaye alianza kupanda  jukwaani tangu alipokuwa sekondari lakini yeye mwenyewe anakiri kwamba mara yake ya kwanza kupanda jukwaani ilikuwa ni wakati wa ufunguzi wa shoo ya mwanamuziki Chaka Chaka pamoja na  Brenda Fassie, wakati wanamuziki  hao kutoka Afrika Kusini ambao walikuja hapa nchini  katika nyakati tofauti tofauti.

Judith Wambura Mbibo au (Lady JD) akiwa katika moja ya shoo zake