TEMBELEA KILA WIKI, SOMA HABARI MPYA. USIKOSE MENGI MENGINEYO WIKI IJAYO. TUPO MAHIRI KUKUHABARISHA PATA VITU VIPYA HAPA. PATA BURUDANI ,HADITHI NA MATUKIO YA MICHEZO KILA JUMA.

Julai 20,1977- Simba 6 Yanga 0

Ilichukua miaka tisa timu ya Simba kulipiza kisasi cha magoli 5-0 dhidi ya Yanga katika mechi ya kuwania ubingwa wa Tanzana iliopigwa Jumanne Julai 20, 1977 kwenye uwanja wa Taifa (Uhuru).

Mahasimu hawa wa jadi walikutana na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0. Magoli yalifungwa na Abdallah Kibaden (dk 25,40,44),  Selemani Saidi Sanga (beki wa kushoto wa Yanga aliyejifunga mwenyewe na (dk 30),Jumanne Hassan Macimental(dk 60,74).

Kikosi cha Simba:
Omary Mahadhi, Daudi Salum, Mohamed Kajole,Aloo Mwitu,
Mohamed Tall, Athumani Juma,Willy Mwaijibe, Aluu Ally, Jumanne Hassan,Abdallah Kibaden na Martin Kikwa/Abbas Dilunga.

Yanga: Yanga: Benard Madale, Charles Boniface, Selemani saidi, Mwanga,Freddy, Jongo, Sam Kampambe, Shabani Katwila, Ezekiel Greyson, Mwinda Ramadhan, Yanga Bwanga na Ayoub/Mrisho Caraby.