Katika historia ya mapambano ya mahasimu wa jadi timu za Simba na Yanga, mchezaji aliyeweka rekodi ya kufunga magoli matatu katika mechi za mahasimu hao ni Abdallah 'King' Kibaden (Chief Mputa).
Kibaden aliweka rekodi hiyo katika mechi iliyochezwa Julai 20, 1977 kwenye uwanja wa Taifa (Uhuru).
Simba ilishinda 6-0, Kibaden alifunga magoli matatu dakika ya 25,40,44.
Abdallah Kibaden (katikati) akiwa katika benchi la wachezaji wa Simba katika moja ya mechi za timu hiyo miaka ya 90. Kulia ni Kocha Msaidizi Etinne Eshete na kushoto ni Daktari Msemakweli