Mshambuliaji anayeminika kuwa kuwa ndiye nyota wa jezi namba 10 hapa nchini katika miaka ya 70, Maulid Dilunga wa Yanga alifanya kejeli dhidi ya mahasimu wao wa jadi Simba.
Dilunga alifunga goli kabla ya mapumziko katika mechi ya fainali ya klabu bingwa dhidi ya Simba ambapo matokeo hadi mapumziko yalikuwa Yanga 1-0.
Dilunga hakurudi uwanjani kipindi cha pili, badala yake alikwenda nyumbani kwa muda, kishaaliporejea uwanjani alikuwa amebadili mavazi na kuvaa suti. Mpira ulipomalizika, Yanga ilishinda 1-0.