Mgogoro mkubwa wa uongozi katika klabu ya Yanga uliosababisha baadhi ya wanachama maarufu wa klabu hiyo wakiongozwa na Mangala Tabu Mangala walijitenga na kujiunga na Nyota Afrika ya Morogoro na baadaye mwaka huo huo kuanzisha Pan Africans.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mwaka huu wa 1986, wachezaji wa kikosi cha kwanza walijiunga na Nyota Afrika ya Morogoro na kuiacha Yanga ikiwa haina wachezaji na hivyo kutolewa hatua za mapema katika ligi.
Mwaka huo Nyota Afrika iliyokuwa na wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Yanga ilicheza fainali na Simba na kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Abbas Dilunga.
Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza waliojiunga na Pan Africans ni Kitwana Manara, Sunday Manara, marehemu Gibson Sembuli, Jellah Mtangwa, Leodger Tenga na wengine wa kikosi cha pili Mohamed Adolph Richard, Juma Pondamali, Mohamed Mkweche, Godian Mapango, Mohamed Tostao, Toto Mokili nk.