TEMBELEA KILA WIKI, SOMA HABARI MPYA. USIKOSE MENGI MENGINEYO WIKI IJAYO. TUPO MAHIRI KUKUHABARISHA PATA VITU VIPYA HAPA. PATA BURUDANI ,HADITHI NA MATUKIO YA MICHEZO KILA JUMA.

1970- West Bromich yafanya ziara Tanzania

Klabu ya West Bromich Albion ya Uingereza ilifanya ziara ya mechi za kirafiki na kucheza na timu za Taifa za Taifa nchi za Afrika Mashariki na kati.

Timu hiyo iliifunga timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars 1-0, Timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars 1-0 na timu ya Taifa ya Uganda The Cranes 1-0.

Kufuatia vipigo hivyo vya timu za taifa, klabu hiyo ilicheza mechi moja zaidi ya kirafiki na timu mchanganyiko ya nchi za Afrika Mashariki.

Katika mchezo huo, timu mchanganyiko ya Afrika ilitoka sare ya bao 1-1, wachezaji wa Tanzania waliochaguliwa katika timu hiyo ni Azizi, Arthur Mambeta, Mbwana, Mohamed  Chuma,  Hassan Chuma na Kitwana Manara. 
Mchezaji  pekee aliyecheza toka Tanzania alikuwa Arthur Mambeta wa Sunderland