Timu ya Yanga ndiyo klabu ya kwanza hapa nchini kushiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika baada ya Tanzania kujiunga rasmi na Chama cha Soka Barani Afrika mwaka 1964.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mashindano ya klabu bingwa Afrika yalianza mwaka 1965 na klabu ya kwanza kufuzu tiketi hiyo ni Cosmopolitans mwaka 1967 ilikuwa bingwa wa Tanzania na kufuzu kushiriki mashindano hayo, lakini ilishindwa kwenda Somalia kutokana na ukata.
Mwaka uliofuata wa 1968 Yanga ilichukua ubingwa na kuifanya Tanzania kushiriki kikamilifu katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza.
1985-Gama aanzisha Majimaji na kutwaa ubingwa wa Tanzania
Timu ya Majimaji ya Songea ambayo ilianzishwa kwa vishindo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, hayati Lawrance Gama na kumchukua mchezaji nyota wa wakati huo, Abdallah 'King' Kibaden kuwa kocha mchezaji wa timu hiyo olifanikiwa kuvifunga vigogo vya Yanga, Simba na Pan na kuchukua ubingwa mwaka 1985.
Mbali ya Kibaden, timu hiyo ilifundishwa na kocha toka Bulgaria, Dimitar Samsarov na baadhi ya nyota kama vile Peter Tino, Octavin Mrope, Sikinde Mbunga na wengineo.