Tanganyika ilijiunga na mashindano hayo ya Gossage mwaka 1945 na kufuatiwa na Zanzibar mwaka 1949.
Nchi nyingine zilizojiunga na kombe hilo ni Malawi na Zambia ambazo hata hivyo zilijiondoa na kujiunga na Shirikisho la Vyama vya Michezo Kusini mwa Afrika (COSAFA) kwa madai kuwa nchi za Afrika mashariki zilikuwa na ushindani mdogo, tofauti na ushindani uliokuwepo kusini mwa Afrika.
Michuano hiyo iliendelea kuzivutia nchi za Ethiopia, Sudan na Somalia ambazo zilijiunga na kuifanya michuano hiyo kupanuka zaidi kutokana na nchi za Afrika Kati kuongeza nguvu.
Aidha, nchi za Rwanda, Burundi, Elitrea na Djibout nazo zilijiunga na kufikisha idadi ya nchi 12.