Ligi ya Muungano ambayo ilizikutanisha mbili zilizofanya vizuri katika Ligi ya Tanzania Bara na ligi ya Tanzania Visiwani kwa ajili ya kupata bingwa wa Muungano.
Ligi hii ilikuwa na mvuto mkubwa ingawa haikudumu kwa muda mrefu ilifutwa baada ya Zanzibar kukubaliwa kuwa mwanachama wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Ligi ya Muungano ya kwanza mwaka 1991 ubingwa ulichukuliwa na Yanga. Yanga ilifanikiwa kuifunga Simba mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya ligi ya muungano, magoli yakifungwa na Athumani China na Abubakary Salum.
Katika mechi ya marudiano ya ligi hiyo ya Muungano Yanga ilishinda tena magoli 2-0 yaliyowekwa wavuni na Saidi Mwamba Kizota dk 41 na 72.
Mwaka huo huo, katika ligi ya Tanzania bara Yanga ilishinda mechi ya kwanza bao 1-0 lililofungwa na saidi Swedi Scud na mechi ya marudiano Saidi Swed Scud akafunga tena 1-0.